Siku chache baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi katika mikoa ya kanda ziwa na kuleta madhara makubwa ambapo mpaka sasa ripoti iliyotolewa ni vifo vya 17 na waliopata majeruhi ni 253, mpaka leo asubuhi kulikuwa na wagonjwa 143′ waliokuwa hospitali.
Leo September 13 2016 serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa imekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, viongozi wa taasisi za umma na binafsi pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa lengo la kukusanya michango itakayosaidia wahanga wa tetemeko hilo.
Waziri Majaliwa ametoa taarifa ya hali halisi ya madhara ya tukio hilo ambalo kwa mujibu wa wanajiolojia, ni tukio la kwanza kusababisha madhara ya kiasi hicho hapa nchini, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ………….
>>>Kwa Tanzania hii ni mara ya kwanza, mara kadhaa tumepata matetemeko madogo dogo, na hasa yanayopita pale kwenye bonde la ufa, lakini hili limekua kubwa na limeleta madhara makubwa, Jambo hili kwa Tanzania ni geni, lakini Lazima tuyapokee’.
>>>’Serikali inajaribu kuona namna ambayo inawasharikisha wadau mbalimbali na nyie mkiwemo. Na mimi nimefarijika sana kwa namna ambavyo mmeomba tukutane hapa ili nyie pia muweze kutoa mchango wenu kwa niaba ya serikali’;-Waziri Mkuu, Majaliwa
ULIKOSA KUTAZAMA HALI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO BUKOBA? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI