Idara ya uhamiaji mkoa wa Pwani imewakamata wahamiaji haramu 43 (Wasomali, Waethiopia na Mbangadeshi) ambao waliingia nchini kinyume na taratibu zilizowekwa.
Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Omary Hassani mkoa wa Pwani kuwa wahamiaji hao walitumia majahazi wakitoka Mombasa mpaka Bagamoyo kwa kutumia bandari bubu ya Lazaba Bagamoyo ambapo walishuka kwenye majahazi na kutembea kwa saa 24 porini mpaka Kijiji cha Kidomole Fukayose Bagamoyo walipoenda kukamatiwa wakisubiri usafiri wa kuwasafirisha kwenda mpakani Mwatanzania ili waendelee na safari yao ya kwenda South Africa.
Aidha Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Omary ameongoza kuwa wanawashikilia Watanzania wanne ambao wanahusika kuwasafirisha wahamiaji haramu hao ambao wote walikamatwa tarehe 6/6/2021 na leo watafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo.