Zaidi ya wiki sita baada ya kuondoka Senegal, manusura 38 wa mkasa wa boti nje ya Cape Verde walirejea Dakar kupitia ndege ya kijeshi Jumatatu jioni, mamlaka ilisema.
Ni miongoni mwa watu 101 walioanza safari tarehe 10 Julai wakijaribu kufika Visiwa vya Canary vya Uhispania.
Zaidi ya watu 60, wengi wao wakiwa wanaume kutoka mji wa wavuvi wa Fass Boye na maeneo jirani, wanahofiwa kufariki, baada ya mashua yao kuelea baharini kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Bado kuna huzuni na hasira katika mji huu baada ya mkasa wa mashua.
Wakazi wachache, wakiwemo watu wa familia moja, waliambia BBC kuwa wamefarijika kujua jamaa zao walikuwa wakirejea nyumbani wakiwa hai.