‘Wahudumu 2,000 wa matibabu’ kaskazini mwa Gaza wanakosa milo ya kufunga Ramadhani
Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa wahudumu wa afya 2,000 wanaofanya kazi katika hospitali katika eneo la kaskazini mwa Gaza lililozingirwa hawakuwa na milo ya kufuturu wakiwa kazini katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.
“Wahudumu wa afya wanakabiliwa na njaa inayoikumba Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza,” msemaji wa Wizara ya Afya Ashraf al Qudra alisema katika taarifa.
Alitoa wito kwa mashirika ya misaada ya kimataifa kuchukua hatua haraka ili kutoa chakula kwa wafanyikazi wa matibabu.