Wizara ya afya imeendelea kutoa elimu Kwa wahudumu wa afya nchini ambapo mara hii Mkoani Morogoro namna ya kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza na magonjwa ta dharulaa Ili kuleta ustawi wa afya.
Akizungunza katika kufunga mafunzo ya siku Tano Kwa wahudumu wa afya kutoka Halmashauri zote za Mkoa Morogoro mkuu wa Kitengo kidogo Cha kukinga na kuthibiti maambukizi nchini amesema serikali inaendelea na kuchukua tahadhari zote za magonjwa ambayo yamekua tishio Duniani Kwa kutoa elimu wataalam hao.
Amesema wahudumu wa afya ni kada muhimu na ndiyo inayoathirika zaidi na magonjwa ambayo yanatoka Kwa wagonjwa kwenda Kwa wahudumu wakati wa kutoa huduma za kitabibu hivyo mafunzo hayo yatakuwa mkombozi kwenye kundi hilo.
Alphonsina Masako afisa muhusika magonjwa yasiyo ambukiza shirika la afya Duniani nchini Tanzania amesema Bado elimu inahitajika
Katika kuendelea kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na ya dharula Kwa wahudumu afya kwani vifo Saba kati ya kumi vinetokana na magonjwa hayo kwenye ukanda wa afrika mashariki.
Naye Christopher Mnzava maratibu amesema wanaendelea kutoa elimu juu ya utambuzi wa magonjwa yasiyoambukiza Kwa wahudumu na Jamii Kwa ujumla.