Mamlaka ya anga ya China imezua mijadala baada ya kutoa maelekezo ya njia nyingine za kupambana na corona kwa kushauri Wahudumu wa Ndege wasiingie vyooni wakiwa angani bali wavae nepi (diapers) ziwasaidie kwenye haja kubwa na ndogo kama Watoto.
Muongozo huo mpya unataka pia Wahudumu wanaosafiri na Ndege kwenda au kutoka kwenye Nchi zenye maambukizi makubwa pia kuvaa kofia za disposable na disposable za viatu.
Pamoja na kwamba wengi wame-maindi huu ushauri wa kuvalishwa nepi, Ripoti moja ya August ilisema Mwanamke mmoja alipata corona kwenye choo cha ndege aliyosafiria kutoka Italy kwenda Korea Kusini ndio sehemu pekee aliingia hajavaa mask na akapata corona.