Boris Johnson anatarajiwa kutangaza mipango ya kuondoa sheria inayowalazimu Watu kuvaa barakoa na hatua ya kuweka umbali kati ya Mtu na Mtu na sasa Waziri huyu Mkuu anasema ataelezea jinsi Nchi hiyo itakavyojifunza kuishi na virusi hivyo.
Kabla ya kukutana na Waandishi wa Habari, Waziri Mkuu Johnson aliashiria kuwa sheria za lazima zitabadilishwa baada ya July 19 siku inayotajwa na Vyombo vya habari vinavyoegemea mrengo mkali wa kulia kuwa ni siku ya ”Uhuru”.
Vizuizi hivyo vitaondolewa katika kipindi cha wiki mbili zijazo licha ya kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo kuongezeka kutokana na kusambaa kwa aina mpya ya kirusi cha corona kiitwacho Delta, mpango huu wa Johnson ni ni tafauti kabisa na mtazamo aliokuwa nao mwanzoni wakati corona ikianza kuitepetesha Uingereza.