Maaskofu,Wainjilisti na Wachungaji wa madhehebu ya kipentecoste na Sabato Tanzania July 13 walikutana kwa ajili ya kuelezea mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa ya nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika 2015.
Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la Jesus Power Miracle Joachim Peter Kimanza wamesema kwa sababu yameshatolewa matamko kadhaa na viongozi kuelekea uchaguzi mkuu na kwa changamoto hizo wamemtolewa mfano Mheshimiwa January Makamba.
Mfano wa January Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia umekuja baada ya kufanya mahojiano na kituo cha BBC London na kutangaza nia ya kuliongoza taifa la Tanzania muda ukifika.
Mbali na kumtaja January Makamba pia wametoa wito kwa vijana wengine wenye sifa za kugombea uongozi huo kujitokeza ili nao wawapime,wawatathmini pamoja na kuwapa ushauri na kuwaombea.