Waandamanaji waliingia mitaani mjini Tel Aviv Alhamisi usiku kuandamana dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu na kutaka kuachiliwa kwa makumi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.
Waandamanaji walibeba picha kubwa za mateka pamoja na ishara zilizo na kauli mbiu, zingine kwa Kiingereza na zingine kwa Kiebrania.
Mwanzoni mwa mwezi huu, makumi ya maelfu ya Waisraeli walikusanyika katikati mwa Jerusalem katika maandamano makubwa zaidi ya kuipinga serikali tangu nchi hiyo ilipoingia vitani mwezi Oktoba. Takriban miezi sita ya mzozo imezusha mgawanyiko juu ya uongozi wa Netanyahu, ingawa nchi hiyo inasalia kuunga mkono vita.
Netanyahu anasema uchaguzi wa mapema utalemaza Israel kwa muda wa miezi sita hadi minane na kusimamisha mazungumzo ya mateka. Ameapa kuwaangamiza Hamas na kuwarudisha mateka wote nyumbani, lakini malengo hayo yameshindikana