RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alioitoa kwa vijana kuweka Mazingira wezeshi ya kufikia ajira laki Tatu.
Lengo la Mhe, Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi lilikuwa kuwaondoa vijana katika utegemezi na kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
Moja ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi katika kipindi cha Miaka Mitatu ni kuongeza kima cha Pensheni jamii kwa Wazee kutoka 20,000 hadi 50,000 sawa na 150%.
Bi. Mwajuma Silima Khamis alisema tunamshukuru Dk.Mwinyi kwa kutuongezea fedha kutoka Elfu 20,000 hadi Elfu 50,000 ambapo fedha hizi zinatusaidia katika mahitaji yetu ya kila siku, tunamuomba Mwenyezi Mungu amzidishie imani kwa kututhamini sisi wazee.
📍Mkaazi wa Koani, Unguja
Moja ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi katika kipindi cha Miaka Mitatu ni kuongeza kima cha Pensheni kwa wastaafu hadi kufikia asilimia 100.
Mzee Iddi Suleiman Jaku naye amesema: tunamshukuru Mh. Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kutufikiria sisi wazee wastaafu kwa kutuongezea kima cha fedha ambapo sasa napokea Shilingi 250,000 kutoka 115,000.
📍Kidimni, Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alioitoa kwa Watumishi wa umma ya kuwaboreshea mazingira mazuri ya Kazi.
Lengo la Rais Dk. Mwinyi ni kuweka mazingira bora ya kazi kwa watumishi wa Serikali na kuongeza ufanisi na uzalishaji.
“Nampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa uamuzi wake wa kutuboreshea mazingira yetu ya kazi ambapo hivi sasa ufanisi wa kazi umeongezeka zaidi na kutoa fursa za ajira nyingine kwa vijana,” Fatma Hassan Haji (43).
📍Fuoni, Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alioitoa kwa vijana kuweka Mazingira wezeshi ya kufikia ajira laki Tatu.
Lengo la Mhe, Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi lilikuwa kuwaondoa vijana katika utegemezi na kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
“Nampongeza Rais wetu Dk.Mwinyi kwa kutekeleza ahadi zake na kuwawezesha vijana kuweza kupata ajira za uhakika kutokana na Mazingira mazuri na wezeshi hivi sasa”– Said Hassan Haji (48).
📍Gulioni, Wilaya ya Mjini, Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu amefanikiwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupata ajira kama alivyoahidi kuzalisha ajira laki Tatu mbali na ajira za muda mfupi.
Mukrim Abdallah Ali, mkaazi wa Meli Nne ambae ni Mfanyakazi wa kiwanda cha Idara Maalum SMZ cha kutengeneza viatu Mtoni amemshukuru Rais Dk.Mwinyi kwa kupata ajira na kuongeza kipato cha uhakika.
“Nilipomaliza kusoma nilikuwa Mtaani tuu, sikuwa na kazi ya msingi ya kufanya wala ujuzi, namshukuru Dk.Mwinyi kwa uwamuzi wake wa kuanzisha viwanda na sasa hivi nina kazi na Ujuzi,” amesema Mukrimu Abdallah Ali (23)
📍MTONI, Unguja