Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo April 11, 2017 amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria ambayo itachunguza mchanga wenye madini uliomo kwenye makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.
Wajumbe walioapishwa ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dkt. Oswald Joseph Mashindano, Bw. Casmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Massawe na Bw. Gabriel Pascal Malata.
Wengine ni Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip ambapo baada ya kuwaapisha wajumbe hao Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyomo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998.
“Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupelekwa nje ya nchi tangu mwaka 1998, na kama hayo makontena yana madini aina ya dhahabu, shaba na silva mkafuatilie tujue zimepelekwa tani ngapi za dhahabu, tani ngapi za shaba na tani ngapi za silva. Je, makontena mangapi yanapita kila mwezi? Makontena 1,000 au mangapi? na, je, zilikuwa na thamani ya kiasi gani? Je, tumelipwa kiasi gani cha fedha?” – Rais Magufuli.
B0nyeza play kutazama hapa chini…
VIDEO: Rais Magufuli amepokea ripoti ya TAKUKURU leo IKULU. Bonyeza play kutazama.