March 4, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson alishiriki ibada takatifu katika kanisa la Jerusalem Temple Sokomatola, Mbeya mjini ambapo pamoja na kushiriki na waumini wenzake katika ibada hiyo Dr Tulia pia alitoa jumla ya shilingi milioni mbili na laki tano kama msaada wake ikiwa Milioni moja kwa ajili ya sikukuu ya wakinamama, Milioni moja na nusu alinunua CD mbili za kwaya katika kanisa hilo.
Pia Dr Tulia alipata fursa ya kushiriki kama mgeni rasmi kwenye Maulid ya wanawake wa kiislam mkoa wa Mbeya iliyofanyika katika msikiti wa Masjid Fyii Sabili Ilah uliopo Forest ambapo alitoa msaada wa misaafu 239 pamoja na juzuu 110 pamoja na kulipia huduma zote ikiwemo chakula ikiwa na lengo la kuwaongezea nguvu ya kielimu katika dini.
“Sisi kama viongozi yawezekana wakati mwingine tukawa hatuwafikii kwa wakati watumishi wa dini lakini mara zote tupo pamoja nanyi na tunatambua sana mchango wenu katika taifa kwa maombi yenu na haswa katika kuwalewa watoto wetu katika maadili mema ambayo yatasaidia kuwa na raia wazuri wenye kumcha Mungu” –Dr Tulia Ackson
Anaedai kugundua Tanzanite aomba kukutana na JPM