Ikiwa bado Afrika Kusini wanaendelea kuchukua vichwa vya habari hususani kupitia muziki wao unaopeta kwasasa kwenye charts mbalimbali.
Sasa taarifa ninayotaka kukupatia ni kwamba Wakali kutokea Afrika Kusini Shakes & Les wanatarajiwa kutumbuiza Julai 22,2023 Jumamosi hii katika Chimbo liitwalo Elements BAR Masaki lilipo Dar es Salaam.
Miongoni mwa ngoma walizowahi kusikika ni hii akiwa Sikisi pamoja na nyinginezo kali zenye rekodi zake. Wakali hao hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwaburudisha Watanzania wanaokoshwa na nyimbo hizo zifahamikazo kwa jina la Amapiano.