Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania imewaondolea hofuwakulima nchini juu ya upatikanaji na bei ya mbolea nchinikwani kampuni hiyo inayo mbolea ya kutosha na itakuwaikipatikana kwa bei nafuu.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa wasambazajimbolea wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, MkurugenziMtendaji wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo alisemashukurani zinaenda kwa serikali kwa kutoa msaada wa ruzukuya bei itakayowezesha upatikanaji wa mbolea hiyo kwa beinafuu.
Kuhusu uwekezaji wa kampuni, Bwana Odhiambo alisemakampuni ya Yara imewekeza kiasi cha dola za Kimarekanimilioni 40 huku kampuni hiyo ikiwa na uwezo wa kuzalishakiasi cha tani laki tano za mbolea kwa mwaka.
“Yara Tanzania inawatoa hofu wakulima nchini kuendelea nashughuli za kilimo bila hofu ya upatikanaji wa mbolea, lakinipia ukiacha soko la Tanzania, pia tunazalisha mbolea kwa sokola Rwanda, Afrika Kusini na Kenya”, alisema.
Akizungumza usajili wa wakulima unaoendelea Meneja waUagizaji na Uuzaji Nje wa Mamlaka ya Udhibiti wa MboleaTanzania (TFRA), Louis Kasera alisema wakulima ambao ndiowalengwa hasa wa mpango huu wa ruzuki wa shs bilioni 150 uliotolewa na serikali ya Raise Samia Suluhu Hassan wanapaswa kuiunga mkono TRFA ili mpango huo uweze kuletatija kwa kwao, waagizaji na wasambazaji.
Naye Meneja wa Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei aliwatakawakulima nchini kuichangamkia huduma yao mpya yaAfricaConect inayowezesha wakulima kupata mikopo yapembejeo za kilimo na viwatilifu kutoka kwa washirika waokupitia Benki ya Equity.
“Tokea tumezindua Africa Connect jumla ya wakulima 50176 wamejisajili kwa Kanda ya Kaskazini huku wakulima 510 wakiwa wameshapata mkopo tukiwa na lengo la kuwafikiawakulima 80,000 nchini kote”, alisema.
Mkutano wa mwaka huu ulitanguliwa na ziara ya wasambazajihao kutembelea kiwanda cha kuzalisha mbolea cha kampunihiyo kilichopo maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
Wakiwa kiwandani hapo wazalishaji hao waliweza kujioneahatua mbalimbali za uzalishaji na ufungashaji wa mbolea na pia kufanya mazungumzo na wataalamu na viongozi wa Yara.
Bwanashamba Mwandamizi Mstaafu wa Yara kiwandanialisema mbolea ya Yara inatengenezwa kwa viwango nakwa kufuata kanuni za ubora za hali ya juu na ndio siri yamatokeo mazuri wanaoyapata wakulima wanaotumiambolea zao.
Naye Kaimu Meneja Idara ya Uzalishaji wa Yara Tanzania, Frank Lugoba akizungumza na wasambazaji hao aliwatakawasambazi hao kufuata taratibu mbalimbali zilizowekwa nakampuni kwa ufanisi wa biashara zao kutoka mbolea inapotokakiwandani mpaka inapowafikia.
Ili kuongeza hamasa kwa wasambazaji hao Yara iliwatangaza, kampuni ya Hapco Agrobusiness mshindi wa kwanza nakujishindia kitita cha shs 58,879,954.84 huku Nasa Kilimowakishika nafasi ya pili wakizawadiwa kiasi cha shs52,674,275.28 wakati Mtewele Traders wakiibuka washindi watatu kwa kujishindia kiasi Cha shs 27,321,514.80.