Siku moja baada ya wakulima wa tumbaku kulalamika kucheleweshewa malipo yao kutokana na ukata wa dola, kampuni ya Alliance One Tanzania Limited ya Morogoro imejitokeza na kuthibitisha kwamba yenyewe imeshawalipa wakulima wote jumla ya dola Milioni 71.9 za kimarekani sawa na Shilingi za kitandania 178.8 Bilioni.
Mkurugenzi wa Alliance One, Ephraim Mappore Amesema wenyewe walifanya jitihada za ziada ili kuwaepusha wakulima na mzigo wa riba ambao wangetozwa na Taasisi za fedha.
Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku(TTB) Stanley Mnozya amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo mpaka sasa wakulima wanadai zaidi ya dola 51 milioni kutoka kwa makampuni yanayotumia zao hilo kama malighafi isipokuwa Alliance One ambao wameshamaliza deni.