Katika kukuza sekta ya Kilimo nchini, Wakulima wametakiwa kutumia fursa za mikopo kupitia Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kutengeneza kipato chenye tija. Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Kanali Shija Lupi ambaye ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT ambao wametoa matrekta manne kwa Wakulima wa Ngano, Kateshi.