Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano vya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wameaswa kuendelea kutangaza majukumu yanayofanywa na taasisi zao kikamilifu ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ama kazi zinazotekelezwa na Taasisi hizo na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bi. Jenita Christian Omolo, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano a Masoko vya Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari lililofanyika katika Ukumbi wa Nanenane, Mkoani Morogoro.
Aliwasisitiza Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wote kutumia jukwaa hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau, na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi utakaoongeza ufanisi katika utendaji kazi a utekelezaji wa maiukumu vao va kila siku kwa maendeleo vao na ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Bi. Omolo alifafanua kuwa Mawasiliano ndio msingi wa mafanikio wa kila jambo, na kupitia mawasiliano Taarifa njema zinazohusu Taasisi zinaweza kusomwa na Wadau mbalimbali wa ndani na nje na kuelewa mambo mazuri wanayoyatekeleza, hivyo wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanazingatia Mawasiliano imara ya kimkakati ili kujenga Taswira chanya kwa Wizara, Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa lengo kuu la kongamano hilo lilikuwa kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazai wa taarifa kwa wadau zinazohusu Wizara na Taasisi zake.
“Nimefarijika sana kuna kwamba mmeitikia wito wa kushiriki katika Kongamano hili, hii ni ishara njema kwa ustawi wa Wizara na Taasisi zake katika kukuza na kumarisha Mawasiliano kwa Umma. Ni matumaini yangu kuwa siku za usoni kongamano hili litakuwa ni miongoni mwa makongamano bora na makubwa zaidi nchini” alisema Bi. Omolo.
Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, aliwapongeza Wahariri na vyombo vya habari nchini kwa namna zinavyosukuma agenda ya Maendeleo na kutangaza habari zinazochagiza ukuaji wa uchumi wa nchi.