Ni Kijana wa kitanzania na Mjasiriamali, Rashid Ally Juma ambae mbali na kwamba ameliteka soko la Ushonaji ‘Suti Bega’ nchini lakini safari hii amekuja na bidhaa nyingine mpya hii ni kwa wale wa maofisini hata wasio wa maofisini.
Chid Designe anasema baada ya soko la ushonaji kufanya vizuri ilimbidi akae na kufikiria biashara nyingine ambayo itamuweka karibu na wateja wake wanaofika na kushona katika kampuni yake.
Akiongea na millardayo.com alisema..’Ikiwa moja ya maono ya kampuni ya Sutibega katika kuhakikisha kila mteja wetu anapata vitu vizuri na vyenye kiwango kinachostahili ili kukamilisha suti za sutibega’- Chid Designer
‘Sasa tumewaletea pen nzuri sana zenye viwango vya juu, kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika maofisi, kazi binafsi, shuleni n.k lakini pia kwa wale wapenzi wa kaunda suti hii pen itafaa sana katika mfuko wa kaunda suti💯 na kukupa urahisi katika kusaini mikataba, kuandika notes zako kwa haraka kwenye vikao mbalimbali bila kuwa na wasiwasi wa kuchafua nguo yako kwa wino’
‘Lakini pia ili kukupa muonekano mzuri wa mfuko wako wa kaunda hivyo usitumie pen za kawaida tumia za peni za #sutibega ili kuonekana nadhifu zaidi💯 na ubora wake ni mkubwa kuanzia material ya nje kwani haichubuki, haivuji wino na ina muonekano mzuri wa umbo la nje’- Chid Designer
‘Pia nitatoa ofa kwa wateja wetu ambao watakuja katika msimu huu kushona suti kwetu basi lazima ajipate peni kutoka kwetu hii ni kuonesha jinsi gani mteja tunamjali na kumthamini’- Chid Designer