Chama cha Walimu Tanzania ( CWT) kimetoa shukrani kwa mhemishiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha kujali maslahi ya watumishi wa umma na kuthamini kazi wanayofanya katika ujenzi wa taifa.
Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro Rais wa CWT,Leah Ulaya amesema kuwa kitendo cha kitendo cha Rais Samia kuonesha anajali maslahi ya watumishi hususan walimu kupitia hotuba yake ya Mei Mosi kimewatia moyo wa kuendelea kujitoa katika utelekelezaji wao wa majukumu yao ya msingi kwa maslahi mapana ya taifa.
Ulaya amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia amefanikiwa ameonesha kwa vitendo kutambua mchango wa walimu na kutambua thamani yao ikiwa ni pamoja na kuwapandisha madaraja,nyongeza ya mishahara,kuboresha miundombinu ya utendaji wao wa kazi na kuajiri zaidi walimu elfu kumi na tatu.
Rais huyo wa CWT amesema kuwa wana matumaini makubwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia kuwa itaendelea kuwaboreshea watumishi mazingira ya kazi na maslahi yao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Chama hicho Maganga Japhet amesema kitendo cha walimu kupewa vishikwambi kimeongeza molali ya kazi na kurahisisha utendaji kazi katika ufundishaji.
Anasema licha ya kupewa vishikwambi lakini pia Rais Samia ameahidi walimu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa hivyo jambo litasaidia sanaa walimu hao.
Naye mmoja wa walimu mwakilishi wa walimu walimu wanawake nchini Elizaberth Werema amesema Rais Samia amendelea kutengeneza mazingira rafiki ya ufundishaji kwa kujenga madarasa ,vyoo ba kuajiri walimu .