Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Morogoro Ndg Mbassah Alphonce ameridhishwa na Umoja unaofanywa na kikundi cha Walimu kupitia kundi lao la Whatsap la Teacher’s Progress we can(TP WE CAN) nchini, Ambapo Kupitia mitandao ya kijamii wa WHATSAP walimu hawa wamekutana na Kutengeneza umoja ambao umekuwa ukiwasaidia hasa nyakati za shida zinapotokea.
Akiwa katika Mkutano Mkuu uliofanyika mkoani Morogoro uliowakutanisha zaidi ya walimu 250 amewapongeza na kusema kuwa katika kufanikisha jambo lolote umoja na kujitoa ndo siri pekee itakayowafanya waweze kupinga wimbi la umaskini na kujiongezea kipato kwa mtu mmoja mmoja au kikundi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Teacher’s Progress We can(TP WE CAN) Mwl.Elias Genge yeye amesema dhumuni kuu la kuanzishwa kwa kikundi hiki ni kuwakutanisha walimu wote nchini na kuwa kitu kimoja lakini pia kushirikiana wakati wa shida zinapotokea kwa mwalimu mmojammoja na mpka sasa zaidi ya walimu 250 wamejiunga na chama hiki kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania
Nao baadhi ya walimu ambao pia ni wajumbe wa chama hiki wameeleza faida ambazo wamezipata kutoka kwa kikundi hiki ikiwemo kuchangia Tsh 5000 kila mwezi lakn wapatapo shida husaidiana na hadi sasa wamefikia zaidi ya Tsh milioni 12.9
Kikundi hiki cha Whatsap cha Teachers Progress we can(TP WE CAN) kilianzishwa na walimu hawa kupitia makundi ya WhatsApp bila wao kujuana na kuanza kuchangia kidogokidogo na leo kwa mara ya kwanza wamekutana mkoani Morogoro kwa lengo la kuendeleza na kudumisha umoja kwa kufahamiana na kutambuana.