Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh amesema idadi ya waliopata madhara kwa kula kiumbe hicho imeongezeka na kufikia watu 160 walioripotiwa na waliofariki ni watoto chini ya umri wa miaka 10 na kufikia idadi ya vifo 9 baada ya 8 walioripotiwa na bado watu 18 kati ya 160 waliopata madhara wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Abdallah Mzee kisiwani Pemba.
Wizara ya afya inapiga marufuku ulaji wa nyama wa kiumbe huyo wa baharini kutokana na kuwa na sumu kali inayotokana na vyakula wanavyokula wakiwa baharini Alisema, kuna aina saba ya kasa na kati ya hizo, nne huwa ni hatari na wana madhara na hafai kuliwa, lakini, ni vigumu kumgundua kasa mwenye sumu kati ya aina hizo saba.
Naye Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Farid Mzee Mpatani, alisema, kasa ana sumu kitaalamu inayoitwa ‘Decarbamoylsaxitoxin’ ambayo inatokana na aina ya majani na matumbawe yaliopo baharini , katika uchunguzi wamegundua sumu hiyo husababisha madhara katika mfumo wa ufahamu wa binadamu na husababishwa na mimea na vimelea vya baharini ambavyo hutumiwa na kasa kama chakula chao.
aidha madhara ya sumu hiyo huleta humsababishia binadamu kukosa nguvu, kupata ganzi, kutapika na kuharisha na kufariki dunia ambapo watoto chini ya miaka 15 huwaathiri zaidi na kuna baadhi ya viumbe baharini wanaweza kula mimea nyenye sumu hiyo na wasilete madhara kwa binadamu, akiwemo kasa na bunju.