Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na kesi ya unyang’anyi kwa kutumia silaha ikiwemo pete ya ndoa yenye thamani ya Sh.Laki 3.
Washtakiwa ni Mussa Kondo (20), Saidi Mashaka (18), Kibwana Nassoro (34) na Ismail Kassim(21).
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Arron Lyamuya na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hamisi Saidi.
Wakili Said alidai kuwa Agosti 28, mwaka huu 2020 katika eneo la Kibamba Njeteni washtakiwa walimnyang’anya vitu mtu aliyefahamika Creny Bagira.
Vitu hivyo ni pamoja na Pete ya ndoa yenye thamani ya Sh.Laki 3 runinga yenye ukubwa wa nchi 40 Sh.850,000, Camera ya Kidigitali aina ya Canon Sh.Laki 6, Fan Make soy sh.60,000, mkoba(hand bag) ambavyo kwa ujumla wake vinakadiliwa kuwa na thamani ya Sh.1,810,000 vikiwa ni mali ya Creny Bagira.
Baada ya kusomewa shtaka hiko, washtakiwa walikana kutotenda kosa hilo, ambapo Wakili Saidi amesema kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wanaomba wapangiwe tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria kosa hilo halina dhamana, hivyo washtakiwa wamerudishwa korokoroni na Hakimu Lyamuya ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 17, mwaka huu 2020.