Polisi Mkoani Shinyanga wanawashikilia Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Mwakitolyo wakituhumiwa kumnywesha pombe Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu huku wakimrekodi na kisha wakarusha video mitandaoni.
“Baada ya video kusambaa Askari wa makosa ya kimtandao waliwasaka na kuwakamata Watuhumiwa akiwemo Baba mzazi wa Mtoto Godius Katisha, Mmiliki wa Baa Irene Pima na Oscar Makondo na watafikishwa Mahakamani upelelezi ukikamilika” -Debora Magiligimba, RPC Shinyanga