Jeshi la Polisi linawashikilia Watu wanane kwa tuhuma za kulishambulia na kulivunja vioo kwa kutumia mawe Bus la Sauli lililosababisha ajali iliyoua abiria mmoja wa Bodaboda Kibaha jana, mawe hayo yalimjeruhi pia Askari.
RPC wa Pwani, Wankyo Nyigesa amekemea vikali tabia ya Wananchi wachache kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira kali kama ilivyotokea katika tukio hilo.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani halitavumilia mihemko ya Watu wachache wasiopenda kutii sheria, tunakusudia kufanya operesheni kali ili kuwakamata wote waliohusika kuharibu na kurusha mawe ambayo pia yalimjeruhi askari Polisi wa Usalama Barabarani aliyekuwa eneo hilo akifanya kazi za kuongoza magari”
“Askari huyo F.3490 SGT Okoka Mbafu amelazwa Hospitali ya Tumbi baada ya kushambuliwa kwa mawe alipofika eneo la tukio kwa ajili ya kuchukua hatua”——— RPC Nyigesa