Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amewasimamisha kazi maafisa wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutokana na tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa zaidi ya Tsh. Milioni 500 katika ukusanyaji mapato, huku akimwagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU0 kufanya uchunguzi mara moja.
Waliosimamishwa kazi ni Innocent Kakuzima ambaye ni Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri hiyo na Beatus Nyarugenda ambaye ni Afisa wa Teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA.
Msimamo wa Dk.Bashiru CCM ‘Siwezi kufanya siasa majukwaani’