TAKUKURU inajiandaa kuwahoji baadhi ya maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini TFF kwa matumizi mabaya ya fedha zikiwemo fedha zilizotolewa na Rais Magufuli Bilioni Moja kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana Afrika, Afcon U17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.
Hata hivyo TAKUKURU imewaamuru maofisa hao wa TFF kurudisha fedha hizo kabla hatua nyingine hazijafata baada ya kupata ushahidi wa nyaraka mbalimbali.