Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atawaapisha Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Taasisi siku ya Jumatano tarehe 19 Mei, 2021 kuanzia saa 4:00 asubuhi badala ya siku ya Jumanne tarehe 18 Mei, 2021 ambayo ilitangazwa awali.
Aidha, Rais Samia atawaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu siku ya Jumatatu tarehe 17 Mei, 2021 kuanzia saa 9:00 Alasiri.
Viongozi hao wataapishwa katika ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam na matukio yote yatarushwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao ikiwemo youtube channel ya Ikulu Mawasiliano na kurasa rasmi za Ikulu Mawasiliano katika Instagram, Twitter na Facebook.