Wakati Mawakala wa Mabasi wakipandisha nauli kiholela kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara ameagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kuwachukulia hatua.
Waitara ametoa maagizo hayo leo alipofanya ziara katika kituo cha mabasi cha Magufuli kuangalia hali ya usafiri wa kwenda mikoani.
Amesema kumekuwa na biashara mbovu ya tiketi na kupandisha nauli kiholela msimu wa sikukuu lakini pia ujanja ujanja wa kuandika nauli tofauti na aliyochajiwa abiria.
“Naelekeza wale wote waliozidishiwa nauli kurudishiwa kumekuwa na tabia abiria kuchajiwa nauli tofauti na iliyoandikwa kwenye tiketi,” Waitara