Watu wawili ambao ni wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuelekea nchini Malawi kuanguka kwenye Mteremko wa wa eneo la Namba One Wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na wandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe ya Makandana walipolazwa majeruhi wa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema watu hao walikuwa wakitokea Nairobi nchini Kenya.
Aliitaja gari waliyokuwa wanasafiria kuwa ni lenye namba za usajiri CA.6439 na tera lenye namba BK. 4744 aina ya Genlyon mali ya Kampuni ya Almeida ya nchini Malawi na kwamba ilikuwa inaelekea mjini Lilongwe.
Kamanda Matei amesema watu hao walikuwa wamejificha chini ya gari hilo kwa kulala juu ya mbao ambazo walikuwa wamezitandika chini ili wasionekane na kwamba gari hiyo ni miongoni mwa magari ambayo Jeshi la Polisi haliruhusiwi kuyakagua.