Katika kuendelea kuthibiti uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na ukusanyaji wa malipo ya watumiaji wa maji Bonde la wami Ruvu ,Wajumbe wa Bodi ya maji bonde la wami Ruvu wamekabidhi bajaji tatu (3) na pikipiki ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi katika kufuatilia uhifadhi wa rasilimali za maji.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti wa bodi ya sita bonde la wami ruvu bi Hafsa Mtasiwa ameipongeza menejiment ya bodi hiyo kwa utendaji kazi mzuri na utekelezaji wa shuhuli zake katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa na kutunzwa na kuwataka wazitumie bajaji hizo kwa matumizi ya ofisi ili ziweze kuleta manufaa kwa Taasisi.
Amesema bodi itaendelea kusimamia masuala yote ya utendaji kazi pamoja na ununuzi wa vitendea kazi ambapo licha ya kutoa vifaa hivyo vya usafiri hivi karibuni wanatarajia kununua magari ya kuendelea kufanya ufuatiliaji wa miradi pamoja utunzaji vyanzo vya maji.
Aidha kwa upande wa mkurugenzi wa bonde la wami ruvu.Mhandisi Elibariki Mmassy amesema vitendea kazi hivyo vimegarimu shilingi milioni thelethini na nane na kwa sasa bodi inasubiri kibali ili waweze kuongeza magari mawili
Mmassy amewataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa kutumia Mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda miti katika maeneo yao kukabiriana na uharibifu wa mazingira .
Katika hatua nyingine Mmassy amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi miradi mbalimbali ikiwemo Mradi mkubwa unaoendelea kwa sasa Bwawa la Kidunda ambalo limegharimu zaidi ya bili 329 ambalo litasaidia upatikanaji wa kwa mikoa mitatu Morogoro,Pwani na Dar es Salaam.