Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu imeadhimisha kilele Cha wiki ya maji Kitaifa kwa Kugawa Miti 3000 Aina ya Mikarafuu katika vijiji vinne Kata ya Kinole Wilaya ya Morogoro Lengo ikiwa ni Kuhifadhi vyanzo vya maji kwa Kuzuia kilimo kisicho na tija katika Vyanzo Vya maji.
Mgeni Rasmi Katika Maadhimisho haya alikuwa ni katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt Mussa Ali Mussa Amesema ‘’ Serikali Itaendelea kutoa miche ya Mikarafuu na Mkoa wa Morogoro utakuwa Sehemu ya Mfano wa Maendeleo ya zao la Karafuu , hivyo Wananchi wa Kinole na morogoro waendelee kupanda miti hii na Kuisimamia mpaka Itakapokuwa.
Aidha Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amesema kuwa Miti ya Mikarafuu ni Miti yenye tija na inasaidia sana kwenye Utunzaji Wa vyanzo vya maji na Kuwataka Wananchi wa Kata ya Kinole kuhakikisha wanapanda miti hiyo na kuitunza vizuri.
Kwa upande wa Chief Kingalu anawashukuru bonde la Wami/Ruvu kuwaletea miti ya mikarafuu kwa sababu wananchi wa kinole wana uhitaji mkubwa wa kupanda miti hiyo na kuwataka wananchi kutoibiana Miti Hiyo.
Hatahivyo kwa Upande wa wananchi wa Kinole wamesema kuwa watahakikisha wanashirikiana vyema Kuhakikisha Miti hiyo inakuwa Vizuri.
Maadhimisho ya Wiki ya Maji yamebeba kaulimbiu isemayo “Uhakika wa maji kwa amani na utulivu.”