Wamiliki wa mabasi mkoani Tanga wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa tozo ya adhabu zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato TRA na Wakala wa usafiri ardhini LATRA kwa wamiliki kushindwa kutoa risiti za kieletroniki kwa wakati kwa abiria wao.
Ombi hilo walitoa wakati wa mafunzo ya matumizi ya tiketi mtandao kwa wanachama wamiliki wa mabasi mkoani Tanga walisema kuwa hatua hiyo inasababisha hasara kwa mmiliki wa mabasi.
Akiongea Mwenyekiti wa Taboa mkoani hapa Abdi Awadhi amesema kuwa licha ya mfumo huo kuwa na manufaa kwa serikali na wamiliki wa mabasi lakini tozo hizo zinatakiwa zingaliwe upya Ili kuweka uwiano sawa .
“Tunaomba serikali iliangali hili la tozo la kushindwa kutoa tiketi mtandao liweze kutozwa na Mamlaka moja badala ya Mamlaka zote mbili kuchukuwa tozo Kwa kosa Moja “amesema Awadhi.
Nae Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Tanga Paul Jackson amesema kuwa lengo mfumo wa tiketi mtandao ni kudhibiti upotevu wa mapato Kwa wamiliki wa mabasi pamoja na serikali Kwa ujumla
“Mfumo huu unakwenda kusaidia serikali kupata takwimu sahihi za vyombo vya usafiri wa ardhini Kwa ajili ya mipango yake lakini na mmiliki wa basi kujua mapato yake stahiki badala ya Sasa ambapo yanapotea”amesema Jackson