Jamii mkoani Morogoro imetakiwa kuondoa dhana ya kutumia dawa bila kupima pindi wanapokutana na changamoto za kiafya kwani kufanya hivyo inahatarisha afya zao kutokana na madhara ya usugu wa dawa unaotokana utumiaji wa dawa mara kwa mara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 30 katika kituo cha huduma za afya cha SUSANNAH WESLEY kilichopo kata ya kihonda maghorofani Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Bahati Faustine amesema watu wengi wamekuwa wakijenga mazoeza ya kutumia dawa pila kupima jambo ambalo huatarisha afya zao kutokana na kuwepo kwa usugu wa dawa mwilini.
Aidha Dkt. Bahati amebainisha kuwa kituo hicho kimejikita katika kutoa huduma kwa gharama nafuu ambapo kukamilika kwa jengo hilo la huduma ya mama na mtoto litasaidia jamii kuondokana adha wanayoipata hasa kwa wamama wajawazito na kuiomba serikali kuwaunga mkono kwa kuwasaidia vifaa tiba na wataalam ili kuweza kutoa huduma kwa ubora zaidi.
Akizindua jengo hilo Afisa tawala Wilaya ya Morogoro Hilali Sagara amepongea hatua ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinaisaidia serikali katika kutoa huduma za kiafya kwa wananchi na kumtaka mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Morogoro kuwashika mkoano ili waweze kutoa huduma hiyo kwa wananchi wengi zaidi.
Hata hivyo akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa halashauri ya manispaa ya Morogoro Dkt. Felista stanslaus ambaye pia ni mratibu wa huduma za afya ndani ya manispaa hiyo amesema wapo tayari kuunga mkono jitihada hizo kwa kutoa baadhi ya vifaa vinavyohitajika.