Leo September 10, 2020 Marekani imetangaza kuwafutia ‘Visa’ Wanafuznzi na Watafiti zaidi ya 1,000 kutoka China ambao wanaodhaniwa kuwa hatari kwa Usalama wa Nchi hiyo.
Hatua hiyo inafuatia tangazo la Rais Donald Trump May mwaka huu akiwalenga Raia wa China wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na Jeshi amesema wengine walikuwa wameiba taarifa na umiliki.
Wizara ya Mambo ya Nje imesema, waliofutiwa ‘Visa’ ni asilimia ndogo ya jumla ya Wanafunzi wa China, na wanaendelea kuwakaribisha wale ambao hawaendelezi malengo ya Chama cha Kikomunisti.
Baadhi ya Wanafunzi wa China nchini humo wanasema wanakabiliwa na uhasama Vyuoni na sababu zao za kusoma zinahojiwa.