Ulishawahi kuendesha usafiri wowote halafu ukakutana na foleni ambayo huwezi kupenya na kutamani kupaa? Ndoto hii inakwenda kuwa kweli baada ya majaribio ya kwanza ya baiskeli inayopaa kufanywa na kufanikiwa huko nchini Japan.
Huu ni mradi wa Wanafunzi wa chuo kikuu cha wazi cha Osaka kupitia ushirika wa Sakai Windmill ambao wamebuni baiskeli inayopaa na kuipa jina “Tsurugi,” wakimaanisha “Upanga” Majaribio ya kwanza yalifanyika katika uwanja wa Nanki Shirahama Airport.
Baiskeli hiyo inayopaa iliyotengenezwa na Wanafunzi ina mabawa na feni kubwa nyuma yake, Mwisho wake unaungana na pedo kumruhusu muendeshaji kuchochea ili kuzidi kwenda na kupaa akiendesha kama zinavyoendeshwa baiskeli za kawaida.
Imeripotiwa kuwa baiskeli hiyo ya kupaa inaweza kusafiri kwa umbali wa Kilomita 19 au Maili 11 za umbali, Ugunduzi huo wa baiskeli ya kupaa umekua maarufu lakini sio wa kwanza kufanyika, Inasemekana kuwa baiskeli ya kwanza ya kupaa ilitengenezwa miaka ya 1880s.
Mwaka 1873 Joseph-Michel na Jacques-Étienne Montgolfier wamerekodiwa kutengeneza puto la hewa la moto ambalo lilikuja kufanyiwa mabadiliko na wabunifu wengine kupunguza baadhi ya vitu na kuongezea vingine kama mashine na pedo za kuendeshea.
April 17, 1889 huko Pennsylvania mbunifu mmoja aliyefahamika kwa jina Altoona Times amerekodiwa kuwa binadamu wa kwanza kufanya majaribio ya baiskeli inayopaa, Tsurugi inaweza kuwa sio baiskeli ya kwanza inayopaa lakini Nchi ya Japan ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na vyombo vya moto vinavyopaa.