Wanafunzi wa vyuo vikuu wameshauriwa Kujikita katika Ujasiriamali ambapo utaongeza kipato chao wawapo vyuoni na baaada ya kumaliza masomo yao.
Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja kitengo Cha ubunifu ujasiriamali na mahusiano ya kitasinia kutoka chuo Kikuu Mzumbe Campus kuu Dr. Emmanuel Chao wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya Kambi ya Ujasiriamali Kwa mwaka huu 2024 katika chuo hicho Campus kuu iliyopo Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Dkt Chao amesema chuo hicho kimekuwa na Utaratibu wa kuandaa wiki ya maonesho ya Ujasiriamali ambayo inafahamika kama kambi ya Ujasiriamali Chuo Kikuu Mzumbe ambapo lengo kuhamasisha wanafunzi Kujikita katika sekta hiyo ili kuongeza Uchumi wao.
Anasema tangu kuanza kwa Kambi hiyo miaka kadhaa iliyopita zaidi ya Wanafunzi mia mbili wamenufaika moja kwa moja ambapo kwa mwaka huu yataanza Machi 20 hadi Machi 22 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Joyce Ndalichako.
Katika Kambi hiyo watu mbalimbali watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao ambapo itakua fursa ya Kuongeza mtaji na wateja na kufahamiana na watu mbalimbali ambapo Chuo Kikuu Mzumbe kitatoa zawadi Kwa wanafunzi watatu watakao leta ubunifu wa kipekee.