Waandishi wa Habari wametakiwa kushirikiana na Jamii inayowazunguka katika masuala mbalimbali ya maendeleo na matendo ya huruma kwa Watu wasiojiweza Ili kujumuika kwa pamoja
Wito huo umetolewa na katibu Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa Morogoro (MORO PC) Bi. Lilian Lucas wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali Kwenye kituo Cha watoto yatima na wenywe ulemavu wa Viungo Cha EMFERD kilichopo kata ya Uwanja wa Taifa Manispaa ya Morogoro.
Liliani amesema mara nyingi Wanahabari wamekua watu wa kuripoti matukio ya watu wengine na wao kujiweka pembeni hivyo waandishi wanawake mkoani humo wameguswa na kununua vitu mbalimbali na kutoa msaada katika kituo hicho ikiwa ni maadhimisho wa siku ya wanamke duniani.
Bi.Lilian Lucas akiongea kwa niaba ya Waandishi wa Habari Wanawake amesema Waandishi wa Habari Wanawake,wanatambua changamoto zinawakabili watu wenye uhitaji kutoka makundi maalum, kuwa pamoja na mahitaji mengine ya kibinadamu wanahitaji upendo ndiyo sababu iliyowagusa kuteua Moja ya kituo kicho.
Lilian alisema kuwa ni muda muafaka kwa Waandishi wa Habari kutumia kalamu zako kuwahamasisha wadau pindi wanapotoa misaada kwa wahitaji wasilenge kwenye vituo vikubwa pekee vinalea makundi maalum hata vituo vidogo ambavyo havina umaalum kwenye jamii.
Akawaomba wadau, taasisi mbalimbali kujitokeza kusaidia kituo hicho kwani mahitaji bado ni mengi kwao na kwamba kimekuwa kikisahaulika na wanaotoa misaada kwa wenye uhitaji.
Kituo Cha Kulelea watoto wenye ulemavu wa viongo na yatima Cha EMFERD kilianzishwa mwaka 2011 baada ya mwanzilishi wake,Bi Josephine Bakita kupata mtoto mwenye ulemavu wa viongo.
Vitu vilivyotolewa na Waandishi wa Habari Wanawake mkoa wa Morogoro ni pamoja na Nguo, Viatu, unga wa Sembe, mafuta ya kula na kupaka,chumvi, juice, pipi, na Maharage.
Kwa Upande wake mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha EMFERD Bi. Josephine Bakita amesema watu wenywe ulemavu na yatima wanahitaji upendo kuliko wali nyama au pilau kwa kuwa maisha kwenye maisha yetu neno upendo ni msamiati mgumu,” amesema Mkurugenzi wa kituo Cha kulelea watoto wenye ulemavu wa viongo na yatima(EMFERD).Bi Josephine Bakita.
Mama Bakita alibainisha hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Wanawake mkoa wa Morogoro walipotembelea kituo hicho katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa Kila mwaka ifikapo Machi 8.
Katika ziara hiyo Waandishi wa Habari Wanawake mkoa wa Morogoro walitoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo unga wa sembe,sabuni,nguo,chumvi na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu