Jeshi la Israel limeanzisha “uvamizi mdogo” zaidi huko Gaza kuwaua watu wenye silaha wa Hamas na kuwatafuta mateka waliochukuliwa kutoka kusini mwa Israel.
Pia ilisema familia za mateka 222 waliothibitishwa ziliarifiwa kuwa wapendwa wao wanazuiliwa katika ukanda wa Gaza.
Idadi “isiyo ndogo” ya raia wa kigeni walichukuliwa mateka na ilikuwa imechukua muda kuwapata, msemaji wa IDF Daniel Hagari aliongeza.
Haya yanajiri huku Rais wa Marekani Joe Biden akiripotiwa kuitaka Israel kuchelewesha mashambulizi ya ardhini katika eneo hilo ili kuachiliwa kwa mateka zaidi.
Wakati huo huo, Israel imezidisha mashambulizi kaskazini mwa Gaza na kuonya mtu yeyote ambaye amesalia yuko hatarini kuchukuliwa kama “mshirika” wa Hamas.
Jeshi la Ulinzi la Israel limesema limeshambulia zaidi ya shabaha 320 huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, zikiwemo miundombinu ya kigaidi na zana za kijes