Video inayovuma kwenye jukwaa la X ambayo zamani ilikuwa ya Twitter ya huko nchini Angola ambayo imepata hisia tofauti ikionesha wakati wanajamii walipokusanyika kumcharaza viboko maiti kwa kuwaibia pesa zao kabla ya kujiua.
Kwa mujibu wa maelezo ya awali kabla ya kupata video hiyo, ilielezwa kwamba mwanamume huyo ambaye ni marehemu alichukua pesa zote kwenye mfuko wa hifadhi ya hela kwa ajili ya jamii.
Baada ya kumaliza pesa hilo kinyemela, jamaa huyo aliona kwamba atagundulika na kutakikana kulipa wakati uwezo wake wa kulipa ni finyu, na hivyo akaamua kujitoa uhai.
Kwa ghadhabu ya wanakijiji katika video hiyo, walimuandalia safari yake ya mwisho vyema lakini kabla ya kumfukia kwenye kaburi, waliamua kumpa funzo la mijeledi mikali kwa kufa na deni lao.
Katika video hiyo inayosambaa, jeneza la marehemu linaonekana kufunguliwa na wanajamii walijipanga wakiwa wamebeba fimbo mikononi mwao ili kumchapa mtu huyo.