Wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al-Shabab Alhamisi walishambulia hoteli maarufu karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi walisema.
Shambulio hilo ambalo al-Shabab ilidai kuhusika, lilianza nyakati za saa tatu na dakika 45 usiku, wakati watu wenye silaha walipovamia hoteli ya SYL kwa risasi nyingi.
“Watu wengi wenye silaha waliingia kwa nguvu ndani ya jengo hilo baada ya kuharibu ukuta wa pembeni kwa mlipuko mkubwa,” afisa wa usalama Ahmed Dahir aliiambia AFP.
Haikufahamika mara moja ikiwa kuna vifo vilitokea.
Mashahidi walielezea kusikia washambuliaji wakifyatua risasi hovyo.