Mashinikizo ya nchi za Magharibi dhidi ya wanamichezo wanaoliunga mkono taifa la Palestina dhidi ya kukiuka sheria za utawala wa Kizayuni wa Israel, yanazidi kuongezeka.
Wamagharibi ambao wanadai kuwa siasa hazipaswi kuingizwa kwenye michezo, sasa wamewageukia wanamichezo wanaopinga ukatili na mauaji ya Israel huko Gaza kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutishia kuwaua wanamichezo hao baada ya kuonesha huruma na mshikamano wao na watu wanaouawa kinyama wa Palestina.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Karim Benzema, mchezaji kanda wa Ufaransa wa timu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia, ni miongoni mwa wale ambao wamekuwa wakilengwa na matokeo yasiyo na kifani ya Wamagharibi wanaouunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel kwa sababu ya uungaji mkono wake kwa watu wanaodhulumiwa wa Palestina.
Seneta wa Ufaransa, Valérie Boyer, ametaka mwanamichezo huyo mashuhuri apokonywe tuzo ya Ballon d’Or na uraia wa Ufaransa kwa sababu tu ya mauaji ya Israel dhidi ya watu wa Palestina.
Benzema aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Dua zetu zote zinawaendea wakazi wa Ghaza, ambao kwa mara nyingine tena ni wahanga wa ushindi wa kinyama ambao hayamwachi mwanamke wala mtoto.”
Kwa upande mwingine, mmoja wa wawakilishi wa Bunge la Ujerumani ametoa wito wa kufukuzwa kwa Noussair Mazraoui, nyota wa soka wa Morocco na mchezaji wa timu ya Bayern Munich ya Ujerumani katika klabu hiyo na Ujerumani kwa ujumla. Wito huo umetolewa baada ya Mazraoui, kulitakia ushindi taifa la Palestina dhidi ya unaouawa watoto wa Israel.
Gazeti la Bild la Ujerumani pia limedai kuwa Noussair Mazraoui anaunga mkono ugaidi baada ya kuwatetea raia wa Gaza wanaouawa na Israel!