Wananchi 260 wakiongozwa na wakili Saimoni mbwambo wamefungua shauri dogo kwenye mahakama kuu kanda ya Tanga dhidi ya halmashauri ya wilaya ya muheza kwa madai ya kutaka kuchukua mashamba yao kuwapa wawekezaji bila kufuata utaratibu .
Awali Wakili saimoni mbwambo akiwawakilisha wananchi hao amesema kua wamefungua shauri hilo dogo kwa wanakijiji 10 ambao watawawakilisha wenzao 250 kutoka vijiji sita ikiwemo mangamlima , mamboleo, zenith, miyanga, vilivyopo tarafa ya bwembera ambapo wanakusudia kufungua shauri la ardhi mahakamani hapo mara baada ya maombi yao madogo ya watu 10 yatakapokubaliwa kuwawakilisha wenzao watapeleka shauri hilo ili kuitaka halmashauri kuacha kuwasumbua wananchi hao ambao wamekua wakitumia mashamba hayo kwa zaidi ya miaka 40 kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na badala yake kama wanayataka ufuatwe utaratibu wa kuwapa fidia inayostahili kulingana na mashamba hayo ambayo ni zaidi heka 1000
Shauri linatarajia kushikilizwa tena tarehe 28 mwezi wa 8 2024 kwaajili hatua zaidi ya shauri hilo.