Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) limesema wananchi 3,600 wamekimbia nchini Ivory Coast kutokana na hofu ya kutokea machafuko baada ya Uchaguzi Mkuu.
UNHCR imesema idadi iliongezeka mara baada ya mchakato wa upigaji kura uliofanyika Oktoba 31 ambapo Rais Alassane Ouattara aliyewania kwa muhula wa tatu alitangazwa mshindi.
Shirika hilo linasema Liberia ambayo inaimarika kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe haina uwezo wa kupokea wakimbizi.