Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amekuatana na watumishi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Bukoba {BUWASA} pamojan na watumishi wa Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini {RUWASA} lengo likiwa ni kuzidi kukumbushana wajibu wao ili kazi zizidi kufanyika kwa ufanisi.
Kupitia kikao hicho kilichofanyika katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera,amewataka watumishi hao kila mmoja kwa nafasi yake kutakiwa kwanza kufahamu majukumu yake yanayotokana na matakwa ya taasisi ili kazi zisiweze kukwama.
“Sisi sekita ya maji lazima tuwe kichocheo cha uchumi,tunatakiwa tusiwe kikwazo katika maisha na kwenye maendeleo,hilo ndo la muhimu kwani wananchi hawahitaji michakato wanahitaji maji” Mhandisi Kemikimba
Kwa upande wao Mkurugenzi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba{BUWASA} John Sirati pamoja na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira Vijijini {RUWASA} Mkoa wa Kagera Mhandisi Warioba Sanya wameahidi kutekeza maelekezo waliyopewa huku wakiwataka wateja wao kuendelea kutoa ushirikiano ili malengo yanayotarajiwa yaweze kufikiwa kwa wakati.