Wakati Dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2000-2025 ikiielekea ukingoni baadhi ya wataalamu Mkoa wa Morogoro wamesema ndani ya miaka 25 taifa limepiga hatua kubwa kwa kufanya mageuzi katika sekta mbalimbali za miundombinu ,elimu pamoja na kuongezeka kwa pato la mwananchi mmoja mmoja.
Dokta Crispian Ryakitimbo ni mjumbe sekretarieti ya maandalizi dira ya taifa ya Mwaka 20250 nasema ilikuwa safari yenye changamoto lakini hatimae taifa limeweza kupiga hatua katika nyanya mbalimbali huku sekta za ujenzi , afya,maji pamoja na elimu zikiwa zimeboreka zaidi ambapo matarajio makubwa kwa baadhi ya wataalamu ni kuelekea dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050.
Katika dira hiyo ya mwaka 2050 wananchi watapata fursa ya kutoa maoni ili kuboresha hali ya miundombinu pamoja huduma kwa jamii kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali.
Kuelekea maandalizi ya Dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 ,baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na makundi ya umma akiwemo Mhe. Jabir Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo amesema taifa limepiga hatua na kuna kila sababu jamii kujivunia mafanikio hayo.
Kwa upande wake kiongozi wa kamati ya uandishi wa dira ya Taifa B 2050 Bw. Maduka Kessy amesema wanatarajia kuzunguka maeneo mbalimbali hapa nchini kuzungumza na viongozi namna ya kukusanya maoni kwa wananchi katika kuboresha dira hiyo.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha huduma bora zinawafikia Wananchi hivyo ushirikishwaji wa wananchi utakuwa na tija kufikia malengo yanayotarajiwa.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesisitiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kupata maoni yatakayo isaidia nchi katika kukua zaidi kiuchumi.
Aidha, ameongeza kuwa dira ya maendeleo ya Taifa ina gusa makundi yote hivyo anatarajia ushirikishwaji mpana wa wadau wote, ngazi zote zikiwemo taasisi za elimu, sekta binafsi, na asasi za kiraia na mwananchi mmoja mmoja.