Wananchi wa Comoro waliotimiza masharti ya kupiiga kura leo wameelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais, huku uchunguzi wa maoni ukionyesha kuwa, Rais wa sasa Azali Assoumani ana uwezekano mkubwa wa kuibuka na ushindi.
Ripoti zinasema, upigaji kura ulianza kufanyika nchini Comoro mapema asubuhi ya leo katika uchaguzi unaotarajiwa kukabidhi muhula wa nne wa miaka mitano kwa Rais Azali Assoumani, ambaye anakabiliwa na wapinzani watano katika kura ambayo baadhi ya viongozi wa upinzani wameisusia.
Wapinzani waliosusia uchaguzi wa leo wanasema kuwa, hakuna mazingira ya kufanyikka uchaguzi huru na wa haki.
Katika uchaguzi uliopita wa mwakak 2029, Tume ya Uchaguzi ya Comoro CENI ilimtangaza Rais Azali Assoumani kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata asilimia 60.77 ya kura, matokeo ambayo wapinzani, asasi za kirai na timu za waangalizi ziliyatilia shaka.