Wananchi wa kata ya Masqharoda wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara wameiomba Serikali kukamilisha Ujenzi wa kituo cha afya walichokianzisha ili kuepuka kufuata huduma za afya umbali wa zaidi ya Km15 katika kituo cha afya Endasaki na hospital ya Dareda-Babati.
Hatua hii ni baada ya ziara ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhandisi Samwel Hhayuma kutembelea kuona hali ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika Jimbo lake, miradi ya elimu,maji, barabara ambapo aliahidi kutoa mifuko 100 ya saruji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya afya katika maeneo yao.
Wananchi hao wamesema ni miaka Mingi wamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya na wakati mwingine wakina mama kujifungulia njiani wakati wakifuata huduma pamoja na kuingia gharama kubwa ya usafiri kufuata huduma.
Hhayuma amesema serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Hanang’ ikiwa ni pamoja na kuongeza watoa huduma za afya na upatikanaji wa dawa.