Wananchi katika Kata ya Nyarugusu Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wamewatuhumu kwa kuwalalamikia Baadhi ya watumishi wa kituo cha afya Nyarugusu Kwa kuomba rushwa kwa Mgonjwa anayekwenda kupata matibabu pkituoni hapo bila kupewa stakabadhi ya Malipo huku wakiomba TAKUKURU kuchunguza watumishi hao.
Wakizungumza katika Mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na Mkuu wa wilaya ya Geita , Hashim Komba wamesema wamechoka na tabia za Baadhi ya watumishi hao ambao wamekuwa wakikiuka Maadili ya kiutumishi ikiwemo kuombwa rushwa ndio wapate huduma .
“Kero yangu ya kwanza ni kuhusu kituo chetu cha Afya huduma ni Hafifu lakini bado rushwa tunaombwa sana hela hapo yaani tunaombwa sana hela hapo hapo kituo cha Afya naomba ulichukue hilo na ulifanyie kazi tuma hata watu wako waje walifanyie uchunguzi yaani ukienda pale kama unaumwa chochote kile kwa mfano mimi kuna mtoto wangu aligombana na mtoto mwingine akachubuka Mkono haka kajitu kakahamia hapa niliombwa hela hapo kama Laki mbili na kitu , ” Bw. Adam.
Kwa upande wake Dkt.Maro William ambaye ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wilaya ya Geita amethibitisha kuwepo kwa watumishi hao Ngazi ya Afya na kukiri kuwachukulia hatua ikiwemo kuwahamisha vituo vyao vya kazi .
” Ni kweli tunakiri kusema kuna changamoto zilijitokeza na hasa zililipotiwa kipindi cha nyuma na Baadhi ya Maamzi yalipelekea ambaye alikuwa ni kinara taratibu za kisheria juu yake lakini pia kwa uchunguzi ambao ulifanyika kwa wakati huo yaliweza kubainishwa moja kwa moja kwa ushiriki ambao ulikuwepo kwa wakati huo , ” Mwakilishi Mganga Mkuu wilaya ya Geita, Dkt.Maro.
Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashim Komba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Geita kuchunguza Tuhuma hizo huku akisema hayuko tayari kuona wananchi wakishindwa kuhudumiwa katika Vituo vyao vya Afya na Kumuagiza Mganga Mkuu wa wilaya kukaa na kujadili kukomesha tuhuma hizo haraka iwezekanavyo.