Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameiomba Wizara ya Nishati kutoa ruzuku ya gesi kwa Wananchi waishio maeneo ya vijijini ili kusaidia utuzwaji wa mazingira na kuthibiti ukatwaji wa miti sambamba na kupunguza gharama pia za maisha wakazi waishio maeneo ya vijijini.
Cherehani ameyasema hayo leoApril 4 bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa —- “Kwenye kata zetu na vijiji hakuna mahala inapouzwa mitungi ya gesi tunaposema tutakuwa na mabadiliko ya utunzwaji wa mazingira na wananchi wote watumie gesi watapata wapi mahala pa kununua gesi na gharama ni kubwa”
“Niiombe Wizara iweke ruzuku kwenye upande wa mitungi ya gesi ili tuwasaidie wananchi wapunguze nguvu ya kukata kuni na tuongeze nguvu kwenye ruzuku” Mbunge Cherehani.