Wizara ya Aridhi nyumba maendeleo ya makazi imetoa siku 30 kwa wamiliki wa aridhi kulipa kodi ya aridhi ndani ya siku husika na watakao kaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza na wanahabari kamishina msaidizi wa aridhi mkoa wa Tanga TUMAINI GWAKISA amesema kuwa ni takwa kishweria kwa wamiliki wa aridhi,makampuni,tasisi na wananchi wote wanao miliki aridhi kwa Tanzania bara kuhakikisha kila mmoaja amelipa kodi ya aridhi ndani ya muda husika wa siku 30.
”Sisi kama kama wataalamu wa aridhi mkoa wa Tanga tutahakikisha tunatoa huduma kwa wakati wote kwanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa mbili usiku ili kuhakikisha tuna wahuduma wananchi ipasavyo,,
Aidha Gwakisa amebainisha kuwa ni wajibu wa wamiliki wote wa Aridhi kuweza kulipa kodi kwani kushindwa kulipa kodi ya aridhi kuna mpelekea mmiliki kuchukuliwa hatua za kisheria .
”Ukishindwa kulipa kodi utachukulia hatua za kisheria na ni kwamba wamiliki wote wana nyaraka za umiliki ambazo kwenye nyaraka za umiliko moja wapo ya mashariti alio pewa nikulipa kodi ndani ya muda wa mwaka mmoja hivyo kulimbikiza kuto kulipa kodi ndani ya mwaka mmoja kuna pelekea kulimbikiza madeni pamoja na riba hivyo kushindwa kulipa kodikwa muda husika inapelekea mamlaka husika kukupeleka mahakamani na kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria hadi kufutiwa umiliki wako kwa mujibu wa sheria,,.
”Kwa wale ambao ni wadai sugu ofisi ina waelekeza watendaji wote wa Halmashauri kwa maafisa aridhi wateule kuhakikisha wana watumia ilani ya siku 14 kwa mujibu wa sheria ,,